Proizvod vam ne odgovara? Nema veze! Proizvode možete vratiti do 30 dana
S poklon bonom ne možete pogriješiti. Za poklon bon primatelj može odabrati bilo što iz naše ponude.
Do 30 dana za povrat
Filamu ni fasihi. Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya filamu na fasihi. Uhusiano huo unatokana na ukamilishanaji wa pande zote mbili kama anavyoelezea Perrier (1992) kwamba, fasihi inatoa mwangaza kuhusu filamu, na filamu inathibitisha thamani ya fasihi. Mtaalamu mwingine ambaye anaonesha uhusiano huo ni Jann (2001) anayeelezea kuwa, filamu kama ilivyo drama na tanzu simulizi kama vile riwaya, zote zinatumia usimulizi ili kufikisha ujumbe kwa hadhira. Hii ina maana kuwa, fasihi (tukichukulia mfano wa riwaya) ina mambo yanayoingiliana na filamu.
Kazi zote zinatumia wahusika, msimulizi, ploti, lugha na mtazamo ili kusimulia hadithi. Katika riwaya, mwandishi anatumia sura wakati kwenye filamu anatumia fremu. Hadhira ya kiriwaya inatumia macho kusoma hadithi, wakati hadhira ya kifilamu inatumia macho kutazama filamu. Kwa hiyo, kuna mwingiliano kati ya fasihi na filamu.
Dobar dan! Ja sam Libroamiko, vaš književni savjetnik.
Kako vam mogu pomoći?